Waluhya

Waluhya (pia: Abaluhya au Luyia) ni kabila kubwa la pili katika Kenya (16% za wakazi wote) wakikalia hasa upande wa Magharibi. Wako pia Uganda na Tanzania. Jumla yao inakadiriwa kuwa milioni 5.3.

Katika Kenya kuna koo 18, Uganda koo 4 na Tanzania ukoo mmoja wa Kiluhya. Koo kubwa zaidi ni Wabukusu, Wamaragoli, Wawanga, Wanyore, Waidakho, Wakisa, Waisukha, Watiriki, Wakabras, Wagisu na Wasaamia.

Kabila Lugha [1] ISO 639-3 Kaunti
Wabukusu Lubukusu bxk Bungoma (Kenya)
Waidakho Luidakho ida Kakamega (Kenya)
Waisukha Luisukha ida Kakamega (Kenya)
Wakabras Lukabarasi lkb Kakamega (Kenya)
Wakhayo Olukhayo lko Busia (Kenya)
Wakisa Olushisa lks Kakamega (Kenya)
Wamaragoli (Waavalogoli) Lulogooli rag Kakamega, Vihiga (Kenya)
Wamarachi Olumarachi lri Busia (Kenya)
Wamarama Olumarama lrm Kakamega (Kenya)
Wanyala Lunyala nle Busia (Kenya)
Wanyole Olunyole nyd Vihiga (Kenya)
Wasamia Lusamia lsm Busia, Kakamega - Uganda
Watachoni Lutachoni lts Kakamega (Kenya)
Watiriki Lutirichi ida Vihiga (Kenya)
Watsotso Olutsotso lto Kakamega (Kenya)
Wawanga Oluwanga lwg Kakamega (Kenya)
  1. Ethnologue: Kiluhya

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search