Wanyakyusa

Nyumba ya asili ya Kinyakyusa,nyumba ya mke wa pili

Wanyakyusa (pia huitwa Wangonde au Wasochile) ni kabila la watu wanaoishi kwenye wilaya ya Rungwe katika sehemu za kusini za Mkoa wa Mbeya (Tanzania), kaskazini kwa Ziwa Nyasa.

Lugha yao, inayoendelea kutumika sana, ni Kinyakyusa.

Mara nyingi Wagonde upande wa kusini wa mto Songwe nchini Malawi huhesabiwa pamoja nao katika kundi lilelile.

Mwaka 1993 watu zaidi ya milioni walikuwa wanajumlishwa kwa jina hili, takriban 750,000 upande wa Tanzania na 300,000 upande wa Malawi.

Mang'oma ni ngoma maarufu ya utamaduni wa Wanyakyusa.

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search