| |||||
Kaulimbiu ya taifa: {{{national_motto}}} | |||||
Wimbo wa taifa: عاش المليك ' ash al-malik "Heri kwa mfalme" | |||||
![]() | |||||
Mji mkuu | Amman | ||||
Mji mkubwa nchini | Amman | ||||
Lugha rasmi | Kiarabu | ||||
Serikali | Ufalme wa Kikatiba Abdullah II Bisher Al-Khasawneh | ||||
Uhuru Tarehe |
25 Mei 1946 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
89,342 km² (ya 112) 0.8 | ||||
Idadi ya watu - Julai 2019 kadirio - 2015 sensa - Msongamano wa watu |
10,407,793 (ya 86) 9,531,712 114/km² (ya 70) | ||||
Fedha | Dinar ya Yordani (JOD )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
UTC+2 (UTC+2) UTC+3 (UTC+3) | ||||
Intaneti TLD | .jo | ||||
Kodi ya simu | +962
|
Yordani, rasmi kama Ufalme wa Kihashemi wa Yordani, ni nchi katika Mashariki ya Kati, inayopakana na Syria kaskazini, Iraq kaskazini-mashariki, Saudi Arabia mashariki na kusini, Israel na Palestina magharibi. Ina idadi ya watu takriban milioni 11.5, ikiwa ya 80 duniani. Jiji lake kubwa zaidi na mji mkuu ni Amman. Yordani imegawanyika katika mikoa 12. Inajulikana kwa mji wa kale wa Petra
Jina la nchi limetokana na mto Yordani ambao ni mpaka wake upande wa magharibi na Israel na eneo la Palestina ya leo.
Jina rasmi ni Ufalme wa Kihashemi wa Yordani (kwa Kiarabu: المملكة الأردنية الهاشمية ) kutokana na familia ya kifalme.
Imepakana na Syria, Iraq, Saudi Arabia, Palestina na Israeli.
Ina pwani fupi kwenye Ghuba ya Aqaba ya Bahari ya Shamu.
© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search